Wednesday 7 September 2016

HADITHI:KILIO CHA MAPENZI SEHEMU YA (1-2)



story: KILIO CHA MAPENZI

mtunzi: long live Josephat.

SEHEMU YA 1


"nilikua nyuma kipindi marafiki zangu wanambaka celina, nilishika condom yangu nisijue la kufanya nilimuonea huruma selina nilisimamisha mishipa ya uoga baada ya kuona damu miguuni mwa celina, nikajisemea moyoni " eeh,  Mungu hivi ni nini kimenifanya niwadanganye wenzangu na kuja kuufanya unyama huu, niliitwa n
a Faridi kwa saut ya chini nilibaki kama zuzu ila nikashtushwa na kofi la uso"...

faridi." we fala ebu fanya haraka tumuache huyu malaya hapa"..

..." faridi alinitaka nimbake celina ili tuondoke tulikua wanne na mm nikawa wa mwisho kwenye tukio lile la kumbaka selina, nilizomewa kwa kuwa muoga kwasababu sehem zangu hazikua na hisia na badala yake wakaniambia nisikubali kumuacha hivi hivi celine nimuingize hata mti kwenye sehem zake za siri ili nimkomoe kwa tabia yake ya kuwa na nyodo wakati naenda kuchukua mti huku nyuma wenzangu wakatoweka wakaniacha mimi na celina ghafla watu wakafika eneo lile na mimi nikafanikiwa kutoka eneo lile, wazo lililokuwa ndani yangu ni kwamba endapo watamuuliza ni nani aliekutenda hivi basi bila shaka mimi nitakua hatiani, nilifika nyumbani nikiwa mpweke sana na mwenye mawazo mengi sikula chakula niliwaza sana,  nilihisi dhambi kubwa moyoni mwangu kwanini nimetenda vile, niliwaongopea wenzangu baada ya kuulizwa kuna msichana gani pale kijijini hua anaringa sana, nikamtaja celina ila moyoni nilimaanisha ni msichana ninaye mpenda sana ila wenzangu waliniunga mkono na kudai kuwa nikweli hua ananyodo sana kwaio walitaka wamfanyie kitu kibaya ndio maana tukawa kwenye tukio la kubaka,.

.." chakushangaza hapakukua na kesi yoyote ile baada ya lile tukio la kubakwa kwa celine tulifurahi sana na hatimaye tukaendelea na maisha yetu.  miaka sita baadae nilienda mjini kutafuta kazi na vibarua vya hapa na pale niliingia kwa njaa kubwa sana mjini  naam maisha hua yanaenda kasi sana nilifikia hatua ya kupata kazi nzuri na maisha mazuri japokua nilikua nakutana na vikwazo vya hapa na pale,

....*" baada ya mwaka mmoja nilifanikiwa kupata mke na nikaoa hatukubahatika kupata mtoto na mke wangu alikua na matatizo ya figo tulihangaika sana ila kilichotakiwa ni figo kutoka kwa mtu mzima mwenye figo nzima laah! sivyo ni kifo kwa mke wangu, nilikubali hali halisi kwasababu sikua na jinsi japo niliumia sana rohoni,  hua wanapita omba omba wengi sana pale ofisini kwangu huwa nawapa siku moja moja siku nyingine siwapi, ila siku hio lilinijia wazo kwanini nisimkamate omba omba, mmoja kisha nikamtoa figo hata kwa bila hiari yake, nilikua mtu mwenye pesa sana sijisifii ila ndio hali halisi, basi haikua shida nilimvizia omba omba wa kike ambae hua anapitaga pitaga sana pale, nilimuita kwa ukarimu kisha nikamkaribisha chakula alikua kachoka ananuka sanaa ila niliigiza ukarimu baada tu ya yule omba omba kumaliza kula hakuchukua muda mrefu akawa amesinzia fofofo.
Nilimtoa nje na kumpakiza kwenye gari kisha nikaenda nae mpaka kwa rafiki yangu faridi ambae alinielekeza jinsi gani nifanye ili nimpate yule omba omba kisha nimpeleke kwa jamaa yake mtaalamu anayeweza kufanikisha zoezi la utoaji figo,  basi nilifika mpaka kwa faridi tukaingia kwenye chumba kikubwa maalumu kwa operesheni ya utoaji figo, hapo nilifanikiwa mke wangu nilimuandaa kwa kila kitu alikua yupo teari eneo lile, nilifanikiwa kuwaweka pamoja na yule omba omba zoezi likaendelea,

utoaji figo ulichukua masaa 12 upimaji na vitu vya kitaalamu vilikuepo madoka mbali mbali walikuemo pia,  hali ikafanikiwa kilichobaki ni kusubiri kuona inavyofanya kazi.

Mke wangu alirudishwa nyumbani na faridi ila yule omba omba nilimpakia kwenye gari yangu nikampeleka kwenye bangaroo langu huko kibamba, nilimtelekeza kwa walinzi wangu na nilifanya hivyo ili akipona tu bas aende zake.

...."baada ya miezi sita mke wangu alipona akapata naafuu yule omba omba nikaona kwake pia ni muda muafaka wa kuondoka kwangu, nikamfukuza kibamba. nilimuona maeneo ya ofisini akiwa anaendelea kuomba omba, sikujali ili mradi tu mke wangu alikua mzima,  niliweka ulinzi mkali kuwa asiingie ofisini kwangu, kuna kipindi alileta fujo kutaka kuingia ofisini kwangu walinzi wangu walimpiga vilivyo na alivuja damu nyingi sana nikaogopa nikahisi wamemtonesha kidonda..... ....



Sehemu ya 2

..." harakati zangu za maisha zinaendelea nikiwa na mke wangu wakati huo nikiwa sijui mbele nini kitatokea ghafla mke wangu akapatwa na ugonjwa wa figo ila nikatatua tatizo lile kutokana na ushauri nilioupata kutoka kwa rafiki zangu"... songa nayo..

..."baada kipindi kirefu kupita tabia za mke wangu zikaanza kubadilika nahisi ni kwasababu ya matatizo waliokuwa wakiyaleta ndugu zangu, mke wangu nilimuoa kimabavu naposema kimabavu namaanisha hakuna mtu yoyote alie ridhia ndoa yetu hasa mama na dada zangu, sikuwa na namna upendo juu ya Agatha ulinitawala nilipoona hakuna wa kuniunga mkono nilirudi nae mjini tukafunga ndoa ya kiserikali, sio wote walinipinga baadhi ya ndugu wa mbali walikuja kujumuika na mimi bas baada ya kukumbuka vikwazo walivyonipa mimi na mke wangu nikagundua fika mke wangu Agatha hua ananuna kwasababu yao na kama mjuavyo ndugu walivyo hasawanapoishi na mtu wasiempenda, alikua ni mama na mjomba ndio nilikua nao pale nyumbani  ikanibidi niwatoe niwapeleke kwenye nyumba ambayo nilikua naimalizia vitu vidogo vidogo iliopo  kongowe,  nilifanya hivyo kuepuka zogo la wazazi wangu na mke wangu. miezi kadhaa ikasogea hali yangu ya kibiashara ikawa sio nzuri hata kidogo nilihangaika huku na kule lakini sikufanikiwa nikamuomba ushauri mke wangu kwakua ni mtu wangu wa karibu na sikua na namna, nilimueleza yotee na kwakweli alinishauri kitu ambacho sikutegemea  aliniambia tukaangalie kwa wataalamu pengine ni tatizo kubwa  nilicheka kisha nikatamka nafsini kuwa "wanawake na mambo haya hawajambo".

.." sikumuamini sana ila nikafanya kwa ajili yake nimuonyeshe kuwa nina jari,  tulifika kwa huyo mganga sehemu ni morogoro  alitufanyia dawa nyingi japo mimi nilijua ni uzushi tu, masharti ni madogo sana na sheria za yule mganga ni kwamba anakupa dawa ya kutatua tatizo baadae ukifanikiwa unarudi anakupa dawa ya kuliroga tatizo pamoja na huyo mtu alietoa tatizo.  nilijua ni mambo ya uongo tu ila nikafanya kwa niaba ya mke wangu, kuhusu malipo, alisema nimlipe nikifanikiwa na malipo ni shilingi elfu mbili.

nilicheka moyoni nikasema " kama ni uongo basi huyu ni mtu ambae anatapeli vitu vidogo sanaa. Tulirudi nyumbani, nikiwa sina imani na ile dawa kuwa itafanya ninyookewe na mambo yangu, hazikupita wiki tatu nikaona mabadiliko makubwa sana nikaanza kuingiza pesa kubwa tena zaidi ya mwanzo nikaanza kuamini kidogo hofu yangu kubwa ikawa ni kwa yule anaenitendea mabaya nikawaza "kama alinifanya niyumbe kiuchumi kwa kuniroga hivi hawezi sasa kuamua kuniua kwa kuniroga ukizingatia nimeshinda vikwazo vyake vya kunididimiza kiuchumi"..

...." niliwaza sana na zaidi na zaidi nilitamani kujua ni nani huyu mtu,  sikukaa na jambo langu moyoni nilienda kumuelezea mke wangu mke wangu akanishauri turudi kwa mganga.  Zilipita siku mbili tukarudi kwa mganga lengo nikujua nani mbaya wangu, mganga alisema ramli ni mbaya na chonganishi sana ila chakufanya atampiga ukoma huyo mtu alie nitenda mimi kwenye biashara zangu, si ukoma kama ilivyo ukoma huu ugonjwa uliozoeleka ila unafanana na ukoma'..

..' sasa ukimpiga ukoma mimi nitamjuaje?"...

." niliuliza swali kwa mganga"..

...."atakuja kuomba msaada kwako siku si nyingi na huyo ndio atakua mwenyewe"..

.." mganga alinijibu huku akiwa makini na uhakika na maneno yake"..

.." imani ya kuamini dawa zake ilinitawala tofauti na mwanzo, mda huu nilimuamini kupita maandiko yoyote wala mtu yoyote,  nilitoa elfu mbili ya tiba kama tulivyoaidiana hapo mwanzo, tulimuaga kisha tukarudi zetu nyumbani"...

.." Baada ya siku tatu nilipatwa na ugeni kutoka kwa mama ugeni ulinishtua sana, mamaangu alikua anaumwa na hakuwezs kushika chochote mikono ikiwa imekakamaa kama mtu mwenye ukoma,nilipata wasi wasi nika yafikiria na kuyatafakari yale maneno ya mganga,  je nikweli mama yangu ndio chanzo cha yale matatizo yangu, sikuamini tena hata kidogo nilimuhifadhi mamaangu pale kwangu asubuhi nikaamkia na safari ya kwenda kwa mganga mimi na mke wangu mama tulimuacha nyumbani na dada,  lengo lakwenda kwa mganga ni kuhakiki kama mama ndie mchawi wangu,   mganga alitoa karai na akaijaza maji kisha akaniuliza unaona nini humu?"

..." maji"..." yule mganga hakuniuliza mpaka pale ilipotokea picha ys mtu ndani ya maji kwenye karai"..

..." huyu unamfahamu?"..

.." niliulizwa na mganga"...

..." ndio namfahamu ni mamaangu"..

..mganga...." huyo ndo alie kuroga nahicho alichoshika ni uchawi hapo kipindi anakuja kwako usiku na kuondoka kimazingara"...


ukose utamu wa sehemu ya tatu na ya nne

itaendelea kesho sehemu ya (3-4)

0 comments:

Post a Comment