Ferooz Ft Juma Nature – Bosi lyrics

 

 

Ferooz
Homa kali imenichachamaa mwilini
Watoto hii wiki ya pili wamefukuzwa ada shuleni
Na mtaani sina amani nimeandamwa na madeni
Mama watoto wahi kazini kwangu upate taarifa 'kama kuna msaada wowote, bosi anaweza kupa...
Alfajiri inayofuata mama akajidaamka 'tukaagana vizuri kazini kwangu akaibuka
Kufika pale bila ya kuipoteza nida, akaingia ofisini nakuanza kueleza shida
Okay, okay, bosi akamkubalia, na fedha akampatia
Kumbe tayari alikuwa ameshamzimia 'ili kumkoleza, fedha akamuongeza
Katika maongezi maongezi mara akamtongoza
Mama akiangalia hali aliyo acha nyumbani 'ni dhiki kubwa ambayo kwakweli hakuitamani
Na kama unavyoelewa mapenzi ya siku hizi
Na alishaahidiwa atagharamiwa yote matumizi
Itabidi akubali tena bila kipingamizi
Baada ya kupita kipindi 'mapenzi yakaanza shamiri, huku kabwela mi sina lile wala hili
Bosi akaanza nipa safari nyingi za kikazi 'ili nikiondoka wapate nafasi ya kumwaga radhi
Hadi kufika hapo mi sikuelewa 'kama kuna picha ninayo chezewa
Wafanyakazi wenzangu wakaja nistua kwamba 'siku hizi wife wangu bosi anamchukua
Kwa kuwa nilimuamini sana wife 'nilibisha, lakini baada ya kuchunguza nikaja hakikisha
Nikamwambia mama watoto ila akakataa, nikimuelezea bwana mkubwa itakuwa kizaazaa, itakuwa kizaazaa...

Chorus
Wanasema, usikubali 'bora niangamie
Wengine wanasema heri nivumilie
Wengine wapi nitapata ajira, niambie?
Na elimu yangu ndio vile mwenzangu na mie
Watoto wataishi kwenye yapi mazingira?
Nikimuambia bwana mkubwa nitaikosa ajira

 

 Ferooz
Taswira yangu ilipoanza kosa muangaza
Na afya ikaanza dhohofika kwa ajili ya kuwaza
Hata muda mrefu haukuchukua 'nikazidi changanyikiwa pale nilipogundua...
Nilipogundua kwamba
La zizi wangu, ua waridi la maisha amebeba mimba kwenye mazingira yaliyo nitatanisha
(?) Ni kama kinda aliokosa wazazi, nikashindwa hata kula wala kupata usingizi, nikawa nakesha...
Kumuomba manani anijalie muelekeo, huku nkivuta subira kusubiri matokeo
Dah, ila sikuamini yangu macho, ilipofika kipindi ambacho 'wife wangu alipojifungua ujauzito
Kuzaliwa mtoto kafanana na yule kizito
Akili ikanituma nichukue panga au rungu ile niende kumdhuru yule mtoto kwa uchungu
Nahisi malaika walipooza jazba zangu na kunikumbusha kuwa kile ni kiumbe cha Mungu
Kupita siku tatu wakaja wafanyakazi wenzangu 'eti kunipa pongezi wakiwa na yule bosi wangu...
Machungu yalinijaa moyoni, lakini nilishindwa kwanza nifanye nini
Nikimuharibia bosi nitafukuzwa kazini, wadhifa wake unafanya apate ninyanyasa Nami kuishi hivyo nafsi yangu inakataa
Nnacho hofia endapo kazi nitaikosa 'watoto wataishi vipi?
Naomba ushauri wa kuufuata
Mwenzenu mimi...
Mwenzenu mimi

Chorus
Wanasema, usikubali 'bora niangamie
Wengine wanasema heri nivumilie
Wengine wapi nitapata ajira, niambie?
Na elimu yangu ndio vile mwenzangu na mie
Watoto wataishi kwenye yapi mazingira?
Nikimuambia bwana mkubwa nitaikosa ajira *2

 

 

 Juma Nature
We Ferooz muharibie (Si ndo hapo)
Muharibie huyo!, mkate kidevu
Bosi mkurugenzi kitambi meneja (Meneja)
Usione tumekonda ukaja ukazania mateja, sa ndio umemfanyia nini mfanyakazi mwenzetu
Si umemchukulia mkewe ndio maana analalamika (Analalamika)
Au kuna lingine Ferooz hataki kuwajibika?
Sikiliza mwanangu Ferooz hapa hatoki mtu (Hatoki mtu)
Nikisema umuache utakuwa umeidhulumu nafsi
Yaani nitajiskia vibaya kwanini huyu bosi hafi 'ameniudhi (Anaudhi)
Ferooz muharibie mzee, mbona una sita,sita? (Una sita, sita)
Embu mkate kidevu mzee, au unamuogopa?
Au nimchape mie, nitamchapa!

Ferooz
Naweza, naweza
Nnachohofia familia kuiteketeza (Nashangaa)
Nyumba nnayo kaa ni mali ya shirika, nitaenda ishi wapi bosi akikasirika
Ukoo mzima mi unanitegemea na mimi kazini pale ndio nilipo egemea
Kutokana na unyama bosi alionitendea, wengine wananishauri eti kwa mganga ninge mwendea

 

Solo Thang
Ferooz basi, hebu tuliza nafsi
Pole sana 'kwa mkasa wa bosi
Tumuombe Mungu aondoe mikosi achana na visasi 'utakuja jijutia
Yaani ishakuwa nuksi ndoa ina ibilisi
Basi, 'Uh-Huh chana karatasi
Talaka tatu sio dawa ya mkosi 'jua unatoa chance ya (?) mikasi
Dhiki, Ibilisi na vichocheo vya bosi mkeo' vilimshawishi aonekane ni muasi, we ubaki na kazi
Uroda alipewa bosi ingawa' kwa nia njema ili wanao wasile nyasi
Yo! Vumilia ni mtihani umepitia 'umshinde shetani hata vitabu vinatuambia
Mungu anasamehe na wewe samehe pia
Kama amekiri kosa 'umkanye asije rudia

Ferooz
Aaah..
Ah, ah, hapana, mm, hapana, hapana, hapana...
Hivyo ndo nitaharibu kabisa, hivyo ndo nitaharibu kabisa...
Nitaishi hadi lini kama mtumwa 'nakosa uhuru wakati hali hiyo kibinafsi ina nidhuru...
Kitu kinacho niongezea mimi majungu kubambikiziwa mtoto ambaye sio damu yangu
Ee mola nisaidie, nipo kwenye janga la utata...
Nipo kwenye janga la utata

[Chorus
Wanasema, usikubali 'bora niangamie
Wengine wanasema heri nivumilie
Wengine wapi nitapata ajira, niambie?
Na elimu yangu ndio vile mwenzangu na
Mie
Watoto wataishi kwenye yapi mazingira?
Nikimuambia bwana mkubwa nitaikosa ajira *2





Comments